Waswahili husema Iso kongwe haivuki na Utu
uzima dawa, misemo hii imedhihirika mwishoni mwa wiki hii wakati
Waziri wa Maliasili na Utalii Mheshimiwa Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) na
timu yake walipomualika Waziri mstaafu wa Maliasili na Utalii Mhe.
Zakia Hamdan Meghji katika uwasilishaji wa bajeti ya wizara hiyo kwa
mwaka 2026/2027 Bungeni Dodoma.
Picha hii inaonesha mkongwe
huyo akiwa na Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Ashatu Kijaji, Naibu
Waziri Mhe. Hamad Chande, Katibu Mkuu Dkt. Hassan Abbasi na naibu
Katibu Mkuu Nkoba Mabula.
Mama Meghji anaheshimika na wizara
ya Maliasili na Utalii kutokana na kuhudumu katika wizara hiyo kwa
kipindi wa miaka tisa (09) iliyosaidia kuchangia mageuzi na
mabadiliko chanya yaliyoimarisha sekta ya utalii, uhifadhi endelevu
wa wanyamapori, misitu na malikale za Tanzania. Kutokana na utumishi
wake uliotukuka katika wizara hii, amewahi kutunukiwa nishani maalum
na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Huyo ndiye Zakia
Hamdan Meghji katika enzi zake akijulikana pia kama “Iron Lady”
wa Tanzania, mwanamke pekee aliyewahi kuwa Waziri wa Fedha kuanzia
mwaka 2006 hadi 2008, na kuwa mwanamke wa kwanza kushika wadhifa huo
nyeti ambapo alifanya kazi kubwa kuimarisha utulivu wa uchumi,
kupunguza umaskini na kusimamia uwajibikaji wa serikali kwenye
masuala ya fedha.

0 Maoni