Wadau wa siasa na waliokuwa wagombea urais nchini wameonyesha kuwa na matumaini makubwa kuwa Tume ya Uchunguzi wa Kijinai iliyoundwa hivi karibuni itatenda haki kikamilifu na kuondoa kabisa hofu na malalamiko ya wananchi kuhusu uwajibikaji.
Tume
hiyo, inayoongozwa na Jaji wa Mahakama ya Rufani Shabani Ally Lila
akisaidiana na makamishna ambao ni majaji wastaafu Gad Mjemmas, Awadh
Mohamed Bawazir, na Aishieli Sumari, inatarajiwa kufanya upelelezi wa
kina ili kubaini wahusika wa ghasia, vifo, na majeraha.
Wadauhao
hao wameeleza kuwa wana imani kubwa na wajumbe hao kutokana na rekodi
zao za uadilifu, wakiamini kuwa watafanya kazi kwa mujibu wa sheria
ili kuleta majibu yataridhisha na kuweka wazi ukweli utakaotibu
majeraha ya kijamii.
Aliyekuwa mgombea urais kupitia Chama cha
Ukombozi wa Umma (CHAUMA), Salum Mwalimu, ameeleza matumaini yake
kuwa kuwepo kwa tume hiyo kutasaidia kuanza kwa uwajibikaji wa kweli,
hatua itakayofanya mioyo ya watu ipoe na kurejesha utayari wa
wananchi kushirikiana kama taifa moja.
Kwa upande wake,
aliyekuwa mgombea urais kupitia Chama cha UMD, Mwajuma Mirambo,
aliongeza kuwa wana matumaini makubwa kwa sababu chombo hicho
kimeundwa na watu sahihi watakaosikiliza maoni ya wanajamii na kuleta
mwarobaini wa jinsi ya kujenga taifa lenye umoja na amani.
Ili
tume hiyo iweze kutenda haki na kufanya kazi yake kwa ufanisi,
viongozi hao wametoa wito kwa Watanzania kuwa watulivu na kuepuka
kuendesha midahalo inayoweza kuingilia au kuvuruga mwenendo mzima wa
uchunguzi huo wa kijinai.

0 Maoni