Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema amani iliyopo nchini ni hazina ya shughuli za kiuchumi na kijamii.
Dkt. Samia amesisitiza kuwa bila amani, hakuna kujenga uchumi wala hakuna shughuli za kijamii.
Dkt. Samia ameyasema hayo leo akizungumza katika kongamano la kitaifa la mama na baba lishe, kwenye ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Mkuu huyo wa nchi, ametumia jukwaa la kongamano hilo, kuwaomba Watanzania kueindeleza amani ya Taifa.
Rais Dkt. Samia amesema kundi hilo linalisha wafanyakazi, wanafunzi, wasafiri pamoja na wananchi kwa ujumla, hivyo kuwezesha shughuli nyingine za kiuchumi na huduma za kila siku kutekelezwa kwa ufanisi.
Aidha, Rais Samia amesema shughuli za Mama na Baba Lishe zinapaswa kutambuliwa na kuheshimiwa kwa hadhi inayolingana na mchango wao katika maisha kila siku ya Watanzania.
Amesisitiza kuwa Mama na Baba Lishe hawapaswi kusumbuliwa wala kunyanyaswa, huku akiahidi kuwa serikali itaendelea kusimamia heshima na ustawi wao.
#KizaziChaAmani


0 Maoni