Rais Mwinyi aridhishwa na maandalizi ya ujenzi wa bandari jumuishi Mangapwani

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema Serikali inaridhishwa na hatua za matayarisho ya ujenzi iliyofikiwa katika mradi wa kimkakati wa Bandari Jumuishi ya Mangapwani.

Dkt. Mwinyi ameyasema hayo leo, tarehe 22 Machi 2026, alipokutana na Mwenyekiti wa Kampuni ya China Harbour Engineering Company Limited, Bw. Bai Yinzhan, pamoja na ujumbe wake waliofika Ikulu, Zanzibar.

Amesema maendeleo ya mradi huo yana umuhimu mkubwa kwa uchumi wa Zanzibar.

Aidha, Rais Dkt. Mwinyi ameeleza kuwa hatua iliyofikiwa kwa sasa inatoa matumaini ya kuona sura halisi ya mradi huo ifikapo mwezi Septemba 2026, ambapo awamu ya kwanza ya mradi inatarajiwa kukamilika.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kampuni ya China Harbour Engineering Company Limited, Bw. Bai Yinzhan, amemuhakikishia Rais Dkt. Mwinyi kuwa kampuni hiyo inaendelea na ujenzi kwa kasi huku ikizingatia viwango vya ubora, ikitambua umuhimu wa mradi huo kwa maendeleo na uchumi wa Zanzibar.

Aidha, amepongeza ushirikiano mzuri wanaoupata kutoka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Rais Dkt. Mwinyi anatarajiwa kuweka jiwe la msingi la mradi wa kimkakati wa Bandari Jumuishi ya Mangapwani leo tarehe 22 Machi 2026.




Chapisha Maoni

0 Maoni