Wakati waumini wa Dini ya kiislam na watanzania kwa ujumla wakisherehekea sikukuu ya Eid al Fitr inayoashiria kumalizika kwa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan ni jambo jema kwa wale wanaotaka kuamini kuwa ipo siku ya mwisho ambapo dunia itakusanywa pamoja na milima yote itakuwa kama mchanga.
Falsafa hii inayozunguzwa na kuhadithiwa ndicho kilichotokea Kreta ya Ngorongoro miaka takribani milioni 2.5 iliyopita.
Katika Quran Tukufu surah ya 99 Surat Az-Zalzalah (Tetemeko la Ardhi) yenye aya 8 inaeleza matukio ya siku ya kiyama ambapo ardhi itatetemeshwa kwa nguvu na kutoa mizigo yake, na wanadamu wataonyeshwa matendo yao, wema au ubaya, hata kama ni ya kiasi cha chembe.
Maelezo ya aya hiyo mfano wake unadhihiri kilichotokea kreta ya Ngorongoro kabla na hali ilivyo sasa.
Wana sayansi wanasema kwamba zaidi ya miaka milioni 2.5 iliyopita ndani ya Kreta ya Ngorongoro wakati Mlima wa Volcano unaodhaniwa kuwa mkubwa kuliko Mlima Kilimanjaro Ulipolipuka.
Mfululizo wa milipuko uliacha uwazi mkubwa ambao haukuweza kuhimili uzito wa kilele chake( koni), hivyo ikaporomoka kuelekea ndani na kuunda kaldera ya volcano mfu yakipekee kubwa zaidi duniani inayojulikana zaidi kama Kreta ya Ngorongoro kulingana na waandishi wa hapo awali.
Kreta hii ina shimo kubwa mithili ya beseni lenye kipenyo cha takriban kilomita 20 na kina cha urefu wa mita 610.
Tukio hili lilitokea wakati wa enzi ya Pleistocene, kipindi kilichoashiria shughuli nyingi hai za volkano katika Bonde la Ufa la Mashariki (Eastern Rift Valley) ni wakati huu ambao bonde la ufa lilikuwa likiongezeka.
Uasili wa eneo hili uliunnda mfumo wa ikolojia unaojitegemea, na kuunda uwanda wa Kreta wenye upekee ukiwa na maziwa ya maji safi na ya chumvi, misitu, nyasi,maziwa, mmito na chemchem miamba inayochomoza na vilima vya kipekee. Mazingira haya yamevutia idadi kubwa ya wanyamapori wa aina mbalimbali, wanaokadiriwa wasiopungua 25,000 kwa vipindi vyote vya Majira ya mwaka.
Historia ya Kreta ya Ngorongoro, ilivyoumbwa na yaliyopo kupitia vitabu takatifu vya dini, ukichanganya na asili, tamaduni, mila na vyote vilivyopo Ngorongoro inadhihirisha kuwa eneo hili ni Bustani ya eden ambapo binadamu, asili utamaduni na vyote alivyoumba mwenyezimungu hadithi zake zote zipo Ngorongoro.

0 Maoni