Wakati nchi ikiendelea na utulivu, matunda ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan yanaendelea kuonekana kupitia utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo inayolenga kutatua kero za wananchi na kuvutia wawekezaji. Hapa, uanaharakati hauna nafasi mbele ya maendeleo yanayogusa maisha ya watu moja kwa moja.
Moja ya matunda ya wazi ni uimarishaji wa usafiri katika
maziwa makuu. Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) hivi karibuni limeripoti
mafanikio makubwa katika Bandari ya Karema, Ziwa Tanganyika. Meli mbili za
mizigo zenye uwezo wa kubeba tani 2,000 kila moja zimeingizwa majini. Hii ni
hatua kubwa itakayochochea biashara kati ya Tanzania, Kongo (DRC), na Burundi.
Miradi hii si tu inarahisisha usafiri, bali inazalisha
ajira kwa vijana na kukuza uchumi wa mikoa ya pembezoni kama Katavi na Kigoma.
Chini ya uongozi wa Rais Samia, Serikali imejielekeza
katika kutekeleza Ilani kwa vitendo, ikilenga kufikia malengo ya Dira ya Taifa
2050 kwa kuhakikisha inaweka mazingira ya uwekezaji sawa kupitia diplomasia ya
kiuchumi. Kwa sasa, Tanzania imekuwa kivutio kikubwa kwa wawekezaji wa
kimataifa (kama ilivyoonekana kwenye mradi wa meli wa Karema), jambo
linaloongeza mzunguko wa fedha na kukuza viwanda.
Aidha ujenzi wa miundombinu ya barabara, reli (SGR), na
nishati ya umeme ni sehemu ya mkakati wa kuhakikisha kila Mtanzania anafurahia
matunda ya uhuru.
Kwa mujibu wa viongozi wa kiroho na wananchi wazalendo,
matunda haya yataendelea kuwa na maana kwa watanzania ikiwa hawatakubali kuingiza uanaharakati au
uchochezi wa maandamano katika mambo ya msingi ya nchi.
Kauli mbiu ya #Hatuandamani imekuwa kielelezo cha utambuzi
wa wananchi kuwa maendeleo yanahitaji utulivu, si fujo.Katika hili Wananchi
wanahimizwa kuendelea kuwa na imani na Serikali kwani nia yake ni njema na
malengo yake ni makubwa kwa ustawi wa wote.
"Usambazaji wa taarifa sahihi unalinda jamii dhidi ya
uvumi na hofu. Tuandike historia ya nchi yetu kwa kufanya kazi, si kwa kupiga
kelele za uanaharakati zinazodidimiza uchumi."
Tanzania inaelekea katika hatua nyingine kubwa ya
kimaendeleo. Kazi ya kuwezesha maendeleo chini ya Rais Samia ni jukumu la kila
mwananchi kwa kulinda amani, kufanya kazi kwa bidii, na kupuuza mianya yote ya
uanaharakati inayolenga kuvuruga utekelezaji wa mipango ya Taifa.
Mabadiliko ya Kiuchumi Katika Bandari ya Karema, kutoka
kuwa na uwezo mdogo wa kuhudumia mizigo mikubwa na usafirishaji ambao
ulitegemea vyombo vidogo ambavyo vilichelewesha biashara na kuongeza gharama za
usafirishaji kwa wafanyabiashara wa mkoa wa Katavi na maeneo ya jirani. hadi
kupata meli kubwa sasa ni hatua ambayo si tu italenda maendeleo lakini
kuwezesha mzunguko wa fedha kuwa mkubwa.
Kwa uwekezaji huu wa Serikali ya Awamu ya Sita, taswira ya
kiuchumi ya Karema inaenda badilika na kuwa lango kuu la biashara ya kimataifa.
Uwepo wa meli hizi sasa unatoa uhakika wa usafirishaji wa bidhaa kwa wingi na
kwa haraka, jambo linalofungua soko la kudumu kati ya Tanzania na nchi za
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Burundi. Hii inamaanisha kuwa gharama za
bidhaa zinapungua kwa mlaji wa kawaida na faida inaongezeka kwa mfanyabiashara,
huku Bandari ya Karema ikigeuka kuwa kitovu cha ajira rasmi na zisizo rasmi kwa
wakazi wa mkoa huo.

0 Maoni