Rais Mwinyi aagiza ZHC kufanya ujenzi wa nyumba za makazi ya wafanyakazi

   

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi ameagiza Ujenzi wa Nyumba za Makaazi ya Wafanyakazi Ufanywe na Shirika la Nyumba la Zanzibar  (ZHC) ili kuongeza Ufanisi katika Ujenzi huo.

Rais DÄ·t. Mwinyi ameyasema hayo leo tarehe 31 Disemba 2025 alipofungua Nyumba za Makaazi ya Wafanyakazi wa Hospitali ya Kitogani, Mkoa wa Kusini Unguja. 

Ameielekeza Wizara ya Afya kujikita katika Ujenzi wa Hosptali na Utoaji wa Huduma za Afya kwa Wananchi badala ya kujenga Nyumba za Wafanyakazi ambalo ni jukumu la Shirika la Nyumba la Zanzibar. 

Rais DÄ·t. Mwinyi ameeleza kuwa Shirika la Nyumba ndilo lenye jukumu la Kuhangaikia Makaazi na Ujenzi wa Nyumba pia lina Uwezo wa kusimamia Ipasavyo, na kutekeleza Ujenzi kwa haraka pamoja na kupunguza gharama.

Akizungumzia Nyumba za Maakazi ya za Wafanyakazi alizozifungua Kitogani amesema lengo ni kuimarisha na kuongeza Ubora wa huduma za Afya kwa Wananchi katika Maeneo yote hapa nchini pamoja na kuwapungizia Masafa Wafanyakazi wa Sekta ya Afya kwa kuwa karibu na jamii wanayoihudumia. 

Aidha, amesema baada ya kufanikisha Ujenzi wa Vituo vya Afya na Hosptali za Wilaya katika Wilaya zote 11hapa nchini ,Serikali inalenga kuhakikisha inakamilisha Ujenzi wa Hosptali za Mikoa katika Mikoa yote Mitano. 

Rais DÄ·t. Mwinyi amefahamisha kuwa Serikali inaendelea na Ujenzi wa Hospitali tatu kubwa za Rufaa ikiwemo Ujenzi Mpya wa Hospitali ya Mnazimmoja, Hospitali ya Matibabu ya Saratani ya Binguni pamoja na Hospitali ya kujifunzia ( Teaching Hospitali ) nayo itakayojengwa Binguni na kueleza kuwa Hospitali hizo zote zitaambatana na Nyumba za Makaazi za Wafanyakazi. 

Akizungumzia Ujenzi wa Nyumba za Makaazi za Kitogani alizozifungua amesena ni Ahadi ya Serikali ya kuwapa Wafanyakazi wa Hospitali hususan Wataalamu Wabobezi Makaazi mazuri na yalio karibu na Maeneo yao ya Kazi. 

Rais DÄ·t. Mwinyi amesema hatua hiyo itazidi kuimarisha Upatikanaji wa huduma za Afya kwa kuhamasisha Wafanyakazi na kupunguza Upungufu wa Nyumba za Maakazi kwa Watumishi wa Umma na tayari Serikali kupitia Wizara ya Afya imejenga Nyumba za Wafanyakazi katika Hospitali nyengine za Wilaya ikiwemo Hospitali ya Abdalla Mzee, Mkoani Pemba. 

Amebainisha kuwa Hatua hiyo ni Utekelezaji wa Ahadi kwa Wananchi wa Zanzibar zilizotolewa wakati wa kuwaomba Kura ili kushirikiana nao katika kutatua Changamoto walizonazo ikiwemo Sekta ya Afya.  

Rais DÄ·t. Mwinyi amesema Serikali itaendelea na miradi mengine kama hiyo ili kufikia Maendeleo Endelevu ifikapo Mwaka 2030 na kuipongeza Wizara ya Afya kwa Kufanikisha Ujenzi huo pamoja na Kumuagiza Mkandarasi kumalizia maeneo yaliobaki katika muda mfupi Ujao. 

Aktoa Taarifa ya Kitaalamu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Nd,Mngereza Miraji Mzee amesema Ujenzi huo wa Jengo la ghorofa 3 uliotekelezwa na Kampuni ya Quality Building Contractor Umegharimu Shilingi Bilionin 5.5 Fedha za Serikali za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar una uwezo wa kuishi familia 16.




Chapisha Maoni

0 Maoni