Kuna
vigezo vitatu muhimu vinavyojenga kiongozi bora wa kijana: Nidhamu, Maarifa, na
Moyo wa Kujitolea.
Haya
yanaonekana katika miktandao katika
majadiliano yanayogusa maisha ya vijana ambao hawataki kuendekeza uchochezi na
kuharibu taifa lao.
Kwa
mujibu wa ujumbe uliopo kwenye mitandao, sifa hizi tatu huunda kijana
anayeheshimika, anayesikilizwa, na anayeweza kuaminika kuliongoza taifa huko
mbeleni.
Ujumbe
huu unafika wakati ambapo Serikali ya Awamu ya Sita, kupitia Ofisi ya Rais
inayosimamia Maendeleo ya Vijana, inaweka mikakati thabiti ya kuwawezesha
vijana.
Hatua
za Serikali za kuwezesha vijana zimethibitishwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais anayeshughulikia Maendeleo ya Vijana, Mhe. Joel Nanauka. Waziri Nanauka
alieleza dhamira ya Serikali katika kuboresha Vituo vya Maendeleo ya Vijana ili
viwe chachu ya kuwawezesha vijana kiuchumi, kijamii na kielimu.
Vituo vikuu vitatu vilivyotajwa na Waziri ni Sasanda (Songwe), Ilonga (Morogoro), na Marangu (Kilimanjaro).
Alikiri
kuwa baadhi ya vituo, kama Sasanda, vilikoma kutoa mafunzo kwa muda mrefu
(tangu 2008), lakini Serikali sasa imejipanga kuviboresha na kuvitumia
kikamilifu ili kuwasaidia vijana katika maeneo hayo.
Alisisitiza
kuwa vituo hivi vina manufaa makubwa kwa vijana katika kuwajengea ujuzi wa
vitendo, ambao ni muhimu katika soko la ajira.
Waziri
Nanauka alikumbusha kwamba Serikali inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu
Hassan imetoa kipaumbele kikubwa kwa vijana, kiasi cha kuunda Wizara maalum
kushughulikia masuala yao.
Hivyo,
vijana wanahimizwa kutambua na kufuatilia kwa karibu mipango hii ya Serikali.
Kwa kutumia vituo hivi, vijana wanaweza kupata ujuzi unaohitajika, kuanzisha
miradi yao wenyewe, na hivyo kutengeneza fursa za ajira kwao na kwa wengine.
Dkt.
Kedmon Mapana, Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais - Maendeleo ya Vijana, naye
alisisitiza umuhimu wa watendaji kutembelea vijana, kufanya kazi kwa kasi, na
kuhamasisha matumizi ya teknolojia katika kutekeleza shughuli za vijana.
Hii
inamaanisha vijana wanatakiwa kujifunza, kujiendeleza, na kutumia fursa
zinazotolewa na Serikali huku wakidumisha sifa za uadilifu ili kuwa tayari
kuongoza taifa kwa heshima na uwezo kesho.

0 Maoni