Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) imeshiriki katika tamasha la Rombo _Marathon lililofanyika leo tarehe 23 Desemba 2025, Rombo Mkoani Kilimanjaro na kuvutia wageni kutoka maeneo mbalimbali ya ndani na nje ya nchi.
Ushiriki wa Ngorongoro Rombo Marathon ambayo pia watumishi wa Mamlaka hiyo wameshiriki mbio za umbali tofauti inadhihirisha jitihada za mamlaka hiyo kuunga mkono sekta ya michezo, kutangaza vivutio vya utalii kupitia utalii wa michezo, kujenga uhusiano na wadau kupitia matukio ya kijamii na kitaifa na kimataifa.
Sambamba na kushiriki
katika tamasha hilo, wananchi waliohudhuria mashindano hayo walipata fursa ya
kutembelea banda la Ngorongoro lililowekwa mahsusi kwa ajili ya kutoa elimu kwa
washiriki na wananchi kwa ujumla kuhusu shughuli za Uhifadhi na utalii
pamoja na mchango wa hifadhi ya
Ngorongoro katika kulinda urithi wa asili na wa kitamaduni.


.jpeg)
0 Maoni