Waziri Mkuu ashiriki Ibada ya Jumapili Usharika wa KKKT Kisasa, Dodoma

 

Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba akisalimiana na Msaidizi wa Askofu  wa Dayosisi  ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dodoma , Mchungaji  Stanley  Tabulu alipowasili kwenye Usharika wa  KKKT Kisasa jijini Dodoma , kushiriki ibada ya Jumapili , Novemba 16.2025. Kulia ni mkewe  Mama Neema Mwigulu Nchemba,  kushoto ni Naibu Spika wa Bunge la Tanzania, Daniel Sllo na wa tatu kulia ni Askofu wa KKKt Dayosisi ya Dodoma,  Askofu Christian Ndosa. 

Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba na mkewe Mama Neema Mwigulu Nchemba wakishiriki katika Ibada ya Jumapili kwenye Usharika wa KKKT Kisasa jijini Dodoma, Novemba 16, 2025. Kulia ni Naibu Spika wa Bunge Daniel Sillo.

Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba akizungumza katika Ibada ya Jumpili aliyoshiriki katika Usharika wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT) Kisasa jijini Dodoma, Novemba 16, 2025.

Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba na Mkewe Neema Mwigulu Nchemba (wa tatu kulia) pamoja na viongozi wengine wakiombewa waliposhiriki katika Ibada ya Jumapili kwenye Usharika  wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Kisasa Dodoma, Novemba 16, 2025.  Kulia ni Naibu Spika wa Bunge, Daniel Siro. (Picha zote na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Chapisha Maoni

0 Maoni