Mtendaji
Mkuu wa Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA), Mhandisi Victor Seff
amesema Serikali ya Tanzania imefanya jitihada kubwa ambayo imeweza kukamilisha
miundombinu iliyoathiriwa na mabadiliko ya tabianchi katika maeneo mengi.
Mhandisi Seff
ameeleza hayo wakati akiwasilisha mada kwenye Mkutano wa Mkutano wa 30 wa Umoja
wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (COP 30) unaoendelea katika Jiji
la Belem nchini Brazil.
Aidha,
katika wasilisho lake Mtendaji Mkuu huyo aliweza kuonesha Makala fupi ya namna
Wakala huo ulivyofanikiwa kurudisha mawasiliano ya miundombinu ya barabara
iliyoharibika kwa kujenga miundombinu himilivu ‘resilient’ kwa athari za
mabadiliko ya tabianchi na zenye uwezo wa kupitika mwaka mzima.
Amesema
kupitia programu ya uondoaji vikwazo katika barabara (bottleneck), wameweza
kujenga madaraja na barabara na hivyo kufungua mawasiliano katika vijiji na
hivyo kuweza kuwasaidia wananchi kusafirisha mazao yao pia kuwarahisishia
kupata huduma za kijamii zikiwemo huduma za afya.
Akichangia
kwenye mradi wa Scale unaosimamiwa na TAMISEMI, amesema TARURA ni mdau mkubwa kwenye mradi huo.



0 Maoni