Mkuu wa Chuo
cha Taifa cha Ulinzi (NDC) Balozi Meja Jenerali W.A. Ibuge ameongoza wakufunzi
na Wanafunzi kutoka mataifa 17, kutembelea eneo la Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA)
kwa kuanzia jengo la makumbusho ya Jiopaki (Urithi Geo- Museum) kwa ziara ya
utalii na kimafunzo.
Ujumbe huo
umejifunza mambo mbalimbali kuhusu vivutio vya utalii, shughuli za
uhifadhi, kijiolojia na urithi wa
utamaduni yanayopatikana katika eneo la Ngorongoro na maeneo yanayozunguka
hifadhi hiyo.
Akizungumza
wakati wa ziara hiyo, Balozi Meja Jenerali Ibuge alisema:
“Tumefurahi
kutembelea makumbusho haya ya kipekee na kisasa ambayo yanaonesha utofauti na
upekee wa Ngorongoro ukilinganisha na maeneo mengine.
Ameupongeza ongozi
wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kwa kazi kubwa ya kulinda rasilimali za wanyamapori, kuendeleza utalii,
na kuchangia kukuza uchumi wa taifa.
Kwa upande
wake, Kamishna wa Uhifadhi Abdul-Razaq Badru, wageni hao amewahakikishia ushirikiano wa karibu kati ya Mamlaka na Chuo
cha Ulinzi cha Taifa na kusisitiza umuhimu wa kuendelea kutembelea hifadhi na
kuwa mabalozi wazuri wa Ngorongoro wanaporudi katika mataifa yao.





0 Maoni