Wito wa uzalendo wa
kweli umepewa kipaumbele, huku wananchi wakikumbushwa kutambua na kuthamini
amani na uhuru wao kama msingi wa maisha ya Taifa.
Gaspar Apolnary
alikumbusha: "Sisi tumeshazoea nchi yetu ni ya amani, tuko na uhuru kila
siku unaenda maeneo yoyote ni salama." Alisisitiza umuhimu wa kuenzi hali
hii: "Tukae kwa amani kwa sababu watu wengi wanategemea kutoka kwetu
)wafanyabiashara)... na hivi kumwezesha kila mtu kufanya shughuli kwa ajili ya
familia yake na taifa."
Shaban Moshi Shaban
alieleza kuwa matendo ya vurugu yaliyoonekana si uzalendo, bali ni uhalifu, na
kwamba maandamano yanapaswa kubeba ujumbe wazi na wa kisheria. "Kitu
wanachokifanya ni kitu ambacho hakifai... waache kufanya hicho walichokuwa
wanakifanya kwa sababu ni uhalifu," alisema.
Uzalendo wa kweli unahusisha
kujenga, kulinda mali za umma na za watu binafsi, na kuepuka vitendo
vinavyovuruga amani na utulivu wa nchi. Kila Mtanzania anahimizwa kudumisha
utulivu na kufuata sheria ili kuendeleza maisha yetu katika mazingira ya amani
tuliyoyazoea.

0 Maoni