Mwenyekiti
wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Mhe. Jaji wa Rufani, Jacobs
Mwambegele ametangazwa majina ya 115 ya wabunge wa viti maalum, huku chama cha
CHAUMMA kikiambulia wabunge wawili wa viti Maalum, CCM ikiwa na wabunge 113.
Jaji
Mwambegele ametangaza majina hayo Jijini Dodoma katika kikao cha tume
alichokiongoza, kikihudhuriwa na Mhe. Jaji wa Rufaa (Mst) Mbarouk Salim Mbarouk
na Katibu wa Tume ambae pia ni Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume, Ramadhani
Kailima.
Katika
orodha hiyo ya wabunge wa viti maalum 115 waliotangazwa tarehe 7 Novemba 2025
Jaji Mwambegele ametaja majina ya wabunge hao wawili wa viti maalum wa CHAUMMA
kuwa ni Devotha Minja na Sigrada Mlingo.
Tume ya
Taifa ya Uchaguzi imesema kwamba inawapongeza wote walioteuliwa kwa nafasi ya
Viti Maalum katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.







0 Maoni