Sauti za wananchi wa
kawaida zimebainisha jinsi vurugu zilivyosimamisha maisha. Familia ziliteseka
na njaa, watoto walikosa shule, na wazazi walishindwa kutekeleza majukumu yao
ya uongozi.
Habib Sadick
anaeleza, kama kiongozi wa familia: "Mimi ni kiongozi katika familia... nina
mke na mtoto, siku tano ni nyingi sana hata kama wewe ni tajiri una fedha
huwezi kuzifanyia chochote kwa kuwa kipindi kile hakina amani hata kidogo.
Maisha tuliyopitia ni funzo."
Salma Juma Kimaro
anaongeza athari kwa jamii: "Mzunguko wetu wa maisha utoke ndio upate
ridhiki. Wengi tumeathirika, watoto shuleni walikuwa majumbani hakuna
chakula."
Haya ni maumivu
yanayotutaka tuimarishe Umoja wa Kitaifa na Mshikamano. Mzee wa Jadi Juma
Mbagho anasema: "Katika mila zetu, tunafundishwa kuketi pamoja baada ya
ghasia. Tusiache chuki ikajenga mizizi. Umoja wetu ndio ngao yetu kuu."
Mbagho anasisitiza
kuwa Taifa linahitaji kuanzisha midahalo ya kijamii inayoongozwa na viongozi wa
kijadi, dini, na serikali ili kujenga imani na kupunguza hofu iliyojengeka
baada ya vurugu.

0 Maoni