Mbunge wa
Jimbo la Mtumba Mh. Anthony Mavunde leo ameshiriki na mamia ya wananchi wa Mtaa
wa Maseya-Kata ya Hombolo Makulu kuanzisha ujenzi wa Zahanati katika mtaa huo
ikiwa ni utekelezaji wa ahadi aliyoitoa wakati wa Uchaguzi Mkuu 2025.
“Nawashukuru
wananchi wa Maseya kwa kumchagua Rais Samia,mimi na Diwani wa kata yetu kwa
kura nyingi sana kwenye uchaguzi mkuu uliomalizika.
Kazi yetu
sasa ni kufanya kazi na kutatua changamoto za wananchi,nawapongeza kwa kuitikia
wito wa ujenzi wa zahanati yetu ambayo itasaidia kusogeza karibu huduma ya Afya
kwa wananchi wetu.
Nitakabidhi
matofali 2000 na saruji mifuko 100 ili kulifikisha juu jengo letu mpaka hatua
ya upauaji,ni imani yangu kwamba serikali yetu sikivu itatuunga mkono
ukamilishaji wa zahanati hii,”alisema Mavunde.
Akitoa
salamu za wananchi,Mwenyekiti wa Mtaa wa Maseya Ndg. Alexander Fwalu
amemshukuru Rais Samia S. Hassan kwa utekelezaji wa haraka wa ahadi ya usambazaji umeme pamoja na uchimbaji wa
visima vya umwagiliaji kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji ambapo wananchi
wengi wakulima watanufaika na kupata maji ya uhakika kwa ajili kilimo cha
umwagiliaji.
Aidha, pia
Mwenyekiti Fwalu amemshukuru Mbunge Mavunde kwa kutimiza ahadi yake ya
kuanzisha ujenzi wa zahanati ya Maseya kwa uharaka na kuahidi kwamba wananchi
wa Maseya watatoa ushirikiano wa kutosha kuhakikisha ujenzi wa zahanati hiyo
inakamilika kwa wakati na hivyo kusogeza huduma ya Afya kwa wananchi.



0 Maoni