Ikiwa ni muendelezo wa maadhimisho ya wiki ya huduma
kwa wateja, Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) limeendelea
kuwashukuru wateja wake wakiwemo makampuni ya utalii, wawekezaji na jamii kwa
ujumla ambao wameendelea kuwa msingi wa uhifadhi na mapato kwa ajili ya
kuimarisha miundombinu mbalimbali ndani ya taasisi na Taifa kwa ujumla.
Kutokana na umuhimu wa wiki hii jana, Oktoba 8,
2025, Hifadhi ya Taifa Kisiwa cha Rubondo imepokea wananchi zaidi ya 40 ambao
ni miongoni mwa wateja wake wakuu waliojielekeza kufanya utalii wa ndani na
kupata elimu ya uhifadhi wa maliasili ikiwemo ulinzi wa mazalia ya samaki.
Wananchi hao ni kutoka katika kata tatu
za wilaya ya Chato ambazo ni Muganza, Bwongera na Kigongo.
Mbali na kufanya utalii wa ndani na kupata elimu ya
uhifadhi pia ziara hii ilijikita zaidi katika kuimarisha mahusiano kati ya
hifadhi na jamii zilizoko pembezoni mwa hifadhi hii, pamoja na kujadili njia
bora za kukuza ushirikiano uliopo baina ya pande hizi mbili ili kufikia lengo
la uhifadhi endelevu wa maliasili na maendeleo ya jamii.
#WikiYaHudumaKwaWateja
#UjiraniMwemaKwaUhifadhi
#TANAPAInaelimisha





0 Maoni