Kumekuwa na maoni tofauti Mtandaoni, mengi yakiunga
mkono kauli ya mmoja wa viongozi wa upinzani
Zitto Kabwe ya kuwataka Watanzania kupuuza wanaotoa wito wa kutopiga kura
Oktoba 29.
Katika klipu ya moja ya hotuba zake katika kampeni
akiwa Songea, Zitto anatoa wito wa wananchi kuwafikiria wanaohimiza kutopiga
kura kama watu wenye walakini ingawa wengine anawaheshimu.
Zitto
Kabwe anayetokea ACT Wazalendo na
mgombea ubunge Kigoma, alisisitiza watu kutoka kwenda kupiga kura kwani
kutofanya hivyo ni kama kununuliwa na chama tawala kukiacha kifanye
kinavyotaka.
Zitto anasema watu wanaohimiza wengine wasishiriki
katika kupiga kura wana walakini vichwani mwao kutokana na umuhimu wa zoezi
hili.
Kauli ya Zitto inachagiza ukweli kuwa kura si tu
haki, bali ni mamlaka ya kuajiri viongozi wa nchi. Kauli ya Zitto imelenga
kuwaamsha Watanzania wachanga kutokubali kupuuzia mchakato huu.
Umuhimu wa uchaguzi unasisitizwa kwa data za vitendo
kwani taifa linatakiwa kuendelea kusonga mbele kijamii na kiuchumi kutoka
katika msingi uliowekwa.
Serikali ya
sasa imewekeza mabilioni ya shilingi katika miundombinu ya kisasa kama vile
Mabasi ya Mwendokasi (BRT), ujenzi wa Hospitali mpya 50 za wilaya, na upanuzi
wa vituo vya afya.
Kwenda kupiga kura Oktoba 29 ni fursa ya kuajiri
Msimamizi: Kura inakupa wewe uwezo wa kuhoji na kuchagua viongozi watakaoweza
kulinda na kusimamia urithi huu wa Taifa, na kuhakikisha huduma bora za afya,
elimu, na usafiri zinasonga mbele.
Aidha ni fursa ya Kudai Uwajibikaji: Vijana
wanahimizwa kuhoji wagombea kwa kutumia sanduku la kura kuhusu changamoto
mbalimbali zinazowakabili wakiwa miongoni mwa wanajamii.
Matusi na uharibifu wa mali za umma (kama vile
mabasi ya BRT na vizimamoto) hauna nafasi katika siasa ya karne ya 21. Kura
yako ni ya ustaarabu na ndiyo njia pekee ya kulinda urithi wa Taifa.
0 Maoni