Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA)
kupitia mradi wa RISE programu ya uondoaji vikwazo katika barabara (bottleneck)
imekalimisha ujenzi wa barabara ya Mtoni-Milo yenye urefu wa Kilomita 5.3
katika halmashauri ya wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani.
Akifafanua juu ya utekelezaji wa mradi huo,
Msimamizi wa mradi huo katika wilaya ya Bagamoyo, Mhandisi Bernard Mwita
ameeleza kuwa mradi huo umekuwa mkombozi kwa wananchi hasa katika shughuli za
kilimo ambazo zilisuasua kutokana na barabara kutopitika.
" Eneo hili lilikuwa halipitiki hivyo
kumalilika kwa mradi huu ni ukombozi tosha kwa wananchi hususani katika
shughuli za kilimo".
Aidha, ameeleza kuwa moja ya kazi katika mradi huo
ilikuwa ni kujenga daraja la midomo mitatu katika eneo lililokuwa korofi ambapo
wananchi walilazimika kuvuka kwa kutumia mtumbwi.
Mmoja wa wakazi wa kijiji cha Geza Ulole, Bw. Joseph
Saidi ameipongeza TARURA kwa kukamilisha utekelezaji wa mradi huo ambao kwao
nikichocheo kikubwa cha uchumi.
Mradi wa RISE sehemu ya uondoaji vikwazo katika
Barabara umetekelezwa kwa awamu ya kwanza katika wilaya ya Bagamoyo mkoani
Pwani ambapo kwa mujibu wa msimamizi wa mradi huo, sehemu ya pili ya
utekelezaji itaendelea kwa lengo la kuondoa vikwazo katika maeneo mbalimbali ya
wilaya hiyo ili wananchi waweze kuzifikia huduma za kijamii.


0 Maoni