Katika mwendelezo wa kuchangia ukuaji wa sekta nyingine kwa maendeleo ya Taifa na Jamii, shughuli za madini katika
Mkoa wa Kimadini Chunya zimechangia ujenzi wa Uwanja wa Mpira wa Miguu wa
Kisasa Wilayani humo kupitia michango ya wadau mbalimbali wa maendeleo wakiwemo
wa Madini chini ya usimamizi ya Halmashauri husika.
Akizungumza katika mahojiano maalum na timu ya
Madini Diary kutoka Wizara ya
Madini, Mjumbe wa Kamati ya maandalizi ya ujenzi wa uwanja huo ambaye pia ni Mkurugenzi
wa KenGold Sports Club Keneth
Mwakyusa amesema kuwa, kujengwa kwa
uwanja huo kunatokana na jitihada
zilizofanywa na Halmashauri ya
Chunya kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wakiwemo wa Sekta ya Madini zilizowezesha kujengwa kwa
uwanja huo wa kisasa wa mpira wa miguu.
“ Tunaweza kusema mapato ya madini pia yamehusika
katika ujenzi wa uwanja kwasababu wadau
waliochangia wapo pia wa madini
ambao wametumia fedha
zilizotokana na na shughuli za madini
lakini wapo na wadau wengine nje ya madini
na usimamizi mkuu umefanywa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Chunya
akisaidiana na kamati ya ujenzi,” amesema.
Ameongeza kwamba, mbali na uwanja huo kutegemewa
kutumiwa na timu za Chunya ikiwemo KenGold unatazamiwa katika siku usoni kutumiwa
kubwa kama Yanga, Simba, Azam na
nyingine huku uwepo wake
ukitarajiwa kuchochea ukuaji wa sekta nyingine kama hoteli, usafiri, chakula na nyingine na
kuongeza kwamba hatua iliyofikiwa hivi sasa ni uwekaji wa nyasi bandia.
Akizungumzia mwenendo wa timu ya Kengold amsema
kwamba timu hiyo bado inaendelea na mazoezi
na wana Imani kwamba itapanda tena daraja na hivyo kutumia
fursa hiyo kuwataka wadau wa michezo nchini wakiwemo wananchi wa Chunya
kuendelea kuiunga mkono timu hiyo.
“Timu yetu
ipo inaendelea na mazoezi, kwa mfano hivi karibuni ilicheza mchezo wa kirafiki
na Songwe na zote zilitoka suluhu ya
mabao mawili kwa mawili 2-2 kwa
hivyo bado tuna imani ya kurejea ligi
Kuu,’’ amesisistiza”.
Naye, Fundi wa uwanja huo Msafiri Napanja amesema
kazi inayoendelea hivi sasa ni uwekaji
wa nyasi bandia iliyopangwa kufanyika ndani ya siku 30 huku maendeleo ya ujenzi
wa uwanja yamefikia asilimia 85.
Awali, akizungumza na timu hiyo ya Madini Diary,
Afisa Madini Mkoa wa Kimadini Chunya Mhandisi Laurent Mayalla amesema kwamba
mchango wa Sekta ya madini wilayani chunya umeyagusa maeneo mengi ikiwemo ya
michezo kutokana na ujenzi wa uwanja
huo.
#Vision 2030:
Madini ni Maisha na Utajiri



0 Maoni