WAZIRI
MKUU, Kassim Majaliwa leo Oktoba 04, 2025 amemwakilisha Mheshimiwa Rais Dkt.
Samia Suluhu Hassan kwenye uapisho wa Rais Mteule wa Malawi, Peter Mutharika
uliofanyika katika uwanja wa Kamuzu, Blantyre nchini humo.
Mheshimiwa
Rais Mutharika wa Chama cha Democratic Progressive (DPP) alimshinda mpinzani
wake Rais Mstaafu Lazarus Chakwera wa The Malawi Congress Party (MCP) kwa
asilimia 56.8.
Mutharika
aliwahi kuwa Rais wa nchi hiyo kati ya mwaka 2014 hadi 2020 alipoangushwa na
Mheshimiwa Chakwera, hivyo Mheshimiwa Rais Mutharika anarudi tena katika kiti
hicho cha Urais baada ya miaka mitano.
Akizungumza
baada ya kuapishwa Mheshimiwa Rais Mutharika amesema nchi ya Malawi ni kwa
ajili ya Wamalawi wote, hivyo amewataka viongozi wajitokeze na washirikiane
katika kuwatumikia watu na si matumbo yao, watoto wao au marafiki zao.
“Sote
tunahitaji mabadiliko na ninawaahidi mabadiliko na kama nchi hii tunataka
kuibadilisha ni lazima yatoke kwetu sisi Wamalawi. Ameongeza kuwa Serikali yake
itahakikisha wananchi wanahudumiwa katika nyanja zote za kimaendeleo na kwa
pamoja tutaijenga Malawi.”


0 Maoni