Naibu
Katibu Mkuu wa Maendeleo ya Jamii Felister Mdemu ametoa amewahimiza maafisa
Maendeleo ya Jamii nchini kuubua fursa za maendeleo katika jamii zao na
kuwajengea uwezo wananchi kuhusu namna ya kunufaika na fura hizo.
Mdemu
amebainisha hayo jana Oktoba 17, 2025 Mkoani Iringa alipotembelea na kukagua
uendeshaji wa miradi katika Chuo cha Maendeleo ya Jamii Rungemba.
Felister
amesema wataalam wa Maendeleo ya Jamii wanatakiwa kwenda mbali zaidi ya kutoa
hamasa peke yake kwa wananchi bali
wanatakiwa kuhakikisha wanawejengea uwezo wa kuweza kunufaika kupitia fursa
wanazoibainisha.
“Wataalam
kutoka Chuo cha Maendeleo ya Jamii Rugemba wamewahamasisha wananchi kushiriki
katika kilimo cha parachichi pamoja na kuwalea katika kila hatua ili waweze
kunufaika na juhudi zao na kujipatia maendeleo,” amesema Felister.
Vilevile
Felister amewapongeza wataalam wa Maendeleo ya Jamii kutoka chuo hicho kwa
kutatua changamoto ya lishe katika Mkoa iringa kupitia ubunifu.
“Pamoja
na Mkoa huu kulima mazao mengi lakini bado kulikia na changamoto ya lishe hivyo Wataalam wa Maendeleo ya Jamii kutoka
Chuo cha Maendeleo Ya Jamii-Rugemba waliweza kubaini mbinu za kuelimisha jamii
ili waweze kuondokana na tatizo hilo,” amesema Felister.
Kwa
Upande wake Mkurugenzi wa Maendeleo ya Jamii Patrick Golwike amesema chuo hicho
kinazidi kutanua wigo wake kwa kuboresha mitaala ili kutimiza dhumuni lake ambalo
ni kutoa wataalam wenye weledi wa kuhudumia jamii na kuleta fursa zenye
manufaa.
“Uboreshaji
wa Mitaala umekuwa ukifanyika kila baada ya muda kupitia ushirikiano wa taasisi
za Maendeleo ya Jamii kupitia kujengeana uwezo na kubadilishana maarifa kwani
kila taasisi ina cha kujifunza kutoka kwa taasisi nyingine, ”amesema Golwike.
Naye
mmoja wa wanufaika wa usimamizi wa miradi unaotekelezwa na Chuo cha Maendeleo ya Jamii-Rugemba Kelvin
Mwaihojo ameishukuru serikali kupitia
chuo hicho kwa kuwekeza juhudi zake na kuwaletea wataalam walioweza
kuwatambulisha katika fursa za kiuchumi na kuwasimamia katika kila hatua mpaka
kufikia mafanikio makubwa.




0 Maoni