Kizazi kipya
kinachoingia kwenye sanduku la kura kina nguvu isiyo na kifani ya kuunda
mustakabali wa Tanzania.
Uchaguzi Mkuu
wa Oktoba 29 si tu zoezi la kisiasa la mara moja; ni mchakato muhimu wa kidemokrasia
unaokupa wewe, kama kijana, jukumu la kubrandi (kuhakikisha utambulisho) na
kuielekeza nchi katika njia unayoitaka.
Wakati maneno
ya "Kura ni haki yako, na amani ni wajibu wako" yakisisitizwa,
umuhimu wako unakwenda mbali zaidi ya kupiga kura tu unahusu kuona mchakato huu
kama chombo cha kujiletea mabadiliko.
Umuhimu wa Kura Yako kwa Kizazi Kipya
Kama injini
ya ukuaji wa taifa, kizazi kipya kinapaswa kuona umuhimu wa kushiriki
kikamilifu katika uchaguzi kutokana na sababu hizi za msingi:
Kuamua Ajira na Uchumi wa Kesho
“ Sisi vijana
ndio wenye changamoto nyingi zaidi. Mimi bado nasoma lakini naona kwamba ajira
ni changamoto. Sasa ni lazima tujue kwa muda mfupi au mrefu nani atasaidia
kuzalisha ajira au hata kutambua kwa hakika kwamba mitaala hii inatusaidia.
Kupiga kura kutasaidia kuingiza watu sahihi kwa ajili yetu” anasema Raphael
Mashilingi.
Vijana ndio
kundi kubwa linalokabiliwa na changamoto ya ajira. Kura yako haichagui tu Rais;
inachagua sera za kiuchumi zitakazojenga viwanda, kuwekeza katika teknolojia
(TEHAMA), na kuongeza fursa za mikopo kwa vijana.
“Nawasihi
vijaa wenzangu twende kumchagua kiongozi ambaye atatoa majibu ya vitendo kuhusu
jinsi atakavyopunguza ukosefu wa ajira na kuwafanya vijana kuwa waajiri, si
waajiriwa” anasema Mashilingi.
Maelezo yake
yanatokana na ukweli kuwa mchakato wa kidemokrasia unakupatia fursa ya kuchagua
mipango inayokidhi mahitaji ya kizazi chako.
Kuunda Utambulisho Mpya (Branding the
Nation)
Kizazi kipya
ndicho cha kwanza kukua kikamilifu katika enzi ya kidigitali. Kushiriki kwako
katika uchaguzi, kwa amani na utulivu, kunatoa picha chanya ya Tanzania kwa
ulimwengu. Unachagua kuifanya nchi yako ibrandiwe kama taifa la Kidemokrasia,
lenye utulivu, na linaloheshimu utawala wa sheria. Utulivu huu ndio huvutia wawekezaji,
na hatimaye, huleta ajira unazozihitaji.
Wajibu Wako:
Zaidi ya 'Kutiki'
Uchaguzi wa
Oktoba 29 unakuhitaji uwe zaidi ya mpiga kura anayekwenda kutiki (kuweka
alama). Unahitaji kuwa balozi wa mchakato wa kidemokrasia.
• Piga Kura na Linda Amani: Amani
Yetu Kwanza haipaswi kuwa kaulimbiu tupu. Kushiriki kwako kunapaswa kuambatana
na kukataa vurugu na matusi ya mitandaoni. Hakuna siasa inayofaa kusababisha
uvunjifu wa amani.
• Chagua Sera, Sio Mihemko: Jikite
katika kuchambua sera na kujua mgombea anasema nini kuhusu afya, elimu, na
ajira. Epuka mihemko, badilisha hisia kuwa uamuzi wenye tija.
Kizazi kipya
ndicho kinaletwa mezani kwa sasa na maamuzi ya nchi hii. Kwa hiyo, toka na
ukapige kura Oktoba 29. Nenda kwa amani, na uonyeshe kuwa kura yako inajenga
Tanzania unayoitaka.

0 Maoni