Kuelekea Uchaguzi Mkuu, Watanzania wameonywa
kutozisikiliza kelele za watu wasioishi nchini wenye lengo la kuvuruga amani na
utulivu wa taifa, huku wakikumbushwa kujifunza kutokana na machafuko
yaliyotokea katika mataifa jirani baada ya vurugu za kisiasa.
Wito huu umetolewa Oktoba 24, 2025 katika moja ya
kampeni za kuuza sera kwa lengo la kuwania kukamata dola, ambapo viongozi
walisisitiza kuwa amani ya Tanzania ndio urithi mkubwa wa taifa, usiopaswa
kuchezewa.
Tahadhari Dhidi ya Propaganda za Kigeni
Imesisitizwa kuwa Watanzania hawapaswi kuvurugwa na
kelele na propaganda zinazotoka nje ya mipaka ya nchi. Wananchi wametakiwa
kuendelea kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama ambavyo vimejipanga
kikamilifu kulinda amani na utulivu wa Taifa kabla, wakati na baada ya Uchaguzi
Mkuu.
Amani imeelezwa kuwa ndiyo msingi wa maendeleo na
ustawi wa Taifa, kwani bila amani hakuna uwekezaji, elimu, afya, wala ibada
zinazoweza kufanyika kwa uhuru.
"Amani inatuwezesha kuabudu kwa uhuru, kufanya
kazi, kuzalisha mali, na kuona maendeleo tunayojivunia leo. Tukilinda amani,
tunalinda maisha yetu na vizazi vijavyo," ilisisitizwa.
Somo Kutoka
kwa Mataifa Jirani
Ili kuonyesha umuhimu wa kulinda amani, Watanzania
wameonywa kujifunza kutokana na historia ya mataifa jirani yaliyopoteza amani.
Mifano ya machafuko hayo ni pamoja na: Kenya (2007): Watu zaidi ya elfu moja
walifariki na zaidi ya laki tatu walipoteza makazi kutokana na vurugu za
kisiasa. Ivory Coast (2010): Watu mia nne na sitini walipoteza maisha kutokana
na machafuko yaliyotokea baada ya uchaguzi.
Imesisitizwa kuwa machafuko haya yameacha somo kubwa
kwa Afrika nzima, kwamba amani ni urithi usiopaswa kuchezewa.
Tanzania itaendelea kuwa kisiwa cha amani na
kimbilio la wengi barani Afrika, endapo wananchi wataendelea kushirikiana
kudumisha hali ya utulivu na mshikamano.

0 Maoni