Mamlaka
ya Hifadhi ya eneo la Ngorongoro (NCAA) kupitia Idara ya Maendeleo ya
Jamii imetembelea kijiji cha Olpiro
kilichopo Kata ya Eyasi, wilayani Ngorongoro, na kuchukua hatua za kutatua
changamoto ya upatikanaji wa maji safi na salama kwa wananchi pamoja na mifugo
yao.
Wataalam
kutoka NCAA katika ziara iliyofanyika
Septemba 30, 2025, wamekagua marekebisho na ukarabati wa miundombinu ya
maji uliofanyika katika kijiji hicho, hatua iliyowawezesha wananchi kupata
huduma ya maji safi na salama.
Ukarabati
wa miundombinu ya huduma ya maji katika
kijiji hicho umeleta faraja kubwa kwa wananchi hao waliokuwa wakikabiliwa na
changamoto ya uhaba wa maji kwa muda mrefu.
Aidha,
pamoja na maboresho ya huduma ya maji, NCAA pia imefanya tathmini ya
miundombinu mingine ikiwemo josho la kuogeshea mifugo lililopo katika kijiji
hicho.
Wananchi
wa kijiji cha Olpiro wameipongeza Serikali kupitia mamlaka ya hifadhi ya
Ngorongoro kwa jitihada hizo wakieleza kuwa zinachangia sio tu katika kuboresha
maisha yao ya kila siku, bali kulinda afya zao na kuendelea kuunga mkono
Serikali katika
shughuli za uhifadhi.



0 Maoni