Mgombea
Ubunge wa Jimbo la Bukombe kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Ndugu Doto
Mashaka Biteko amewahimiza wananchi wa Kata ya Butinzya, Wilayani Bukombe
kumpigia kura mgombea wa Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM)Dkt.
Samia Suluhu Hassan ili aendelee kuongoza na kusimamia miradi ya maendele iliyokwishaanzishwa
na hivyo kuwaletea maendeleo.
Dkt.
Biteko amesema hayo Septemba 30, 2025 wakati wa mkutano wa kampeni katika Kata
ya Butinzya wilayani Bukombe mkoani Geita ikiwa ni sehemu Kampeni za Uchaguzi
Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani utakaofanyika Oktoba 29, mwaka huu.
Amesema
wananchi wanalo jukumu la kujotokeza kwa wingi kupiga kura na watakapopiga kura
maana yake ni kutimiza wajibu wao kidemokrasia ambao utawawezesha kutimiziwa
mahitaji yao kwa kujengewa miradi ya maji, umeme, barabara, hospitali na shule.
Amesema
katika miaka mitano iliyopita wananchi hao wakishiriki katika kutekeleza miradi
ya maendeleo iliyolenga kutatua changamoto za Bukombe na sasa jukumu lililopo
mbele ni kuboresha na kuongeza miundombinu kwa maslahi mapana ya wananchi wa
Wilaya ya Bukombe na Taifa kwa ujumla.
“Kipindi
kilichopita hapakuwa na barabara lakini leo tumeifungua miundombinu ya barabara
kutoka Butinzya hadi Isemabuma na maeneo mengine. Changamoto ya maji
tunaifanyia kazi na tutahakikisha yatapatikana katika umbali usiozidi mita 400,
tunajenga zahanati nyingine na tunataka kuongeza madarasa na kukarabati shule,”
amesema Dkt. Biteko.
Ameongeza
maendeleo yaliyopatikana ni uwezeshaji kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan “ Haya yote anayoweza kuyafanya ni
Dkt. Samia, mimi siwezi kufanya haya yote bila msaada na uwezeshaji wake.
Hivyo, niwaombe wananchi wote 7,111 mliojiandikisha mjitokeze na kumpigia kura
Dkt. Samia.”
Akiendelea
na kampeni zake katika Kata ya Igulwa, Dkt. Biteko amesema kuwa Rais Samia
amedhamiria kuleta maendeleo katika Wilaya ya Bukombe kwa kuendelea kujenga
barabara za lami ambapo barabara ya Ushirombo kwenda Katoro imeanza kujengwa.
Pia,
amesema Rais Samia ametoa kibali kwa ajili ya kuchimba madini katika Pori la
Kigosi ili kuwasaidia wananchi hapo kujipatia kipato.
Dkt.
Biteko amebainisha kuwa katika Shule ya Sekondari Bukombe kupitia ufadhili wa
Ubalozi wa India wanajenga kituo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano ili
wanafunzi wa Bukombe waweze kuwa na elimu ya masuala ya teknolojia kwa manufaa
yao.
Kwa
upande wake, Naibu Katibu Mkuu Umoja wa Vijana Taifa wa Chama Cha Mapinduzi
Tanzania Bara na Mjumbe wa Halmashauri Kuu, Mussa Mwakitinya amesema Ilani ya CCM inaweka wazi malengo ya Serikali
kukuza uchumi wa Mtanzania na kuongeza ustawi wa jamii.
“ Ilani
yetu imeeleza hapa kuwa Dkt. Samia ana mpango wa kumuona kila Mtanzania ana
maisha mazuri, anatenga bilioni 99 kwa ajili ya wanawake na shilingi bilioni 96
kwa ajili ya vijana. Hapa Bukombe CCM italeta shilingi bilioni 2 kwa ajili ya
mikopo,” amesema Mwakitinya.
Naye,
Mgombea wa Udiwani Kata ya Butinzya, Kwizi Mathias amewaeleza wananchi hao kuwa
endapo watawachagua wagombea wa CCM Oktoba 29 watahakikisha wanafanyia kazi
changamoto chache zilizopo katika Kata hiyo ikiwemo upatikanaji wa maji.
Kwa
upande wake, Mgombea Udiwani wa Kata ya
Igulwa, Richard Mabenga amewaomba wananchi hao kuendelea kumuamini na kumchagua
tena katika nafasi ya udiwani.
Aidha,
amesema waichague CCM kwa kuwa pamoja
na miradi mingine wamejenga shule ya sekondari ya Dkt. Biteko, sekondari ya
amali ya Igulwa iliyogharimu shilingi milioni 580.
Sambamba
na hayo wameanza kujenga mtandao wa
barabara za lami , wamechimba kisima, wamejenga Chuo Kikuu hivyo Oktoba
29 wananchi wawachague wagombea wa CCM.




0 Maoni