Mgombea ubunge wa Arusha Mjini
kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Paul Makonda, amekiri kuwahi kulishwa sumu
hali iliyomsababishia kulazwa hospitalini na kutoonekana hadharani.
Makonda amefichua siri hiyo leo
Jumapili, Septemba 21, 2025, wakati wa ibada katika Kanisa la Mbingu Duniani
lililopo Njiro, Arusha, akisema si mara yake ya kwanza kulishwa sumu na kwamba
amenusurika kifo mara kadhaa.
“Kuna kipindi nilipotea nikaanza
kutafutwa, na wengine mlinitafuta kwa nguvu kubwa huyu yuko wapi. Ukweli
nilikuwa naumwa, nililishwa sumu,” alisema Makonda.
“Yasingekuwa maombi ya Watanzania
na Mungu kumuinua Rais Samia Suluhu Hassan kusimamia matibabu yangu nilitakiwe
nife mwaka jana,” amesema Makonda.
0 Maoni