Katika
kuadhimisha Siku ya Faru Duniani, wananchi wa mji wa Karatu wameungana na
Maafisa wa Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), Askari wa Jeshi la Polisi Wilaya ya
Karatu, pamoja na wadau mbalimbali wa uhifadhi na utalii kushiriki mbio maalum
za kilomita tano zenye lengo la kuhamasisha juhudi za uhifadhi wa mnyama Faru.
Maadhimisho
hayo, yaliyoandaliwa na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kwa kushirikiana na
taasisi mbalimbali, yamefanyika leo Septemba 22, 2025 huku yakiongozwa na kaulimbiu isemayo:
“Tuhakikishe aina tano za Faru waliopo duniani wanaishi.”
Katika
maadhimisho ya Siku ya Faru Duniani Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro inafanya
shughuli mbalimbali ikiwepo kutoa elimu ya uhifadhi wa Faru kwa jamii, kutoa
elimu ya utunzaji wa mazingira, maonesho ya uhifadhi wa Faru pamoja na Michezo
mbalimbali yenye lengo la kuhamasisha uhifadhi wa Faru.
0 Maoni