Makatibu Wakuu wanaoshughulikia Maliasili na Utalii Afrika Mashariki wamekutana Jijini Arusha kwa lengo la kukamilisha maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Mawaziri wa sekta hiyo kutoka nchini zinazo unda Jumuhia ya Afrika Mashariki (EAC) unaotarajiwa kufanyika leo tarehe 12 Septemba 2025 Jijini Arusha.
Akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili
na Utalii nchini, baada ya kikao hicho kilichojumuisha wataalam wa Uhifadhi
kutoka nchi za Jumuhia hiyo, Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii anaeshughulikia Uhifadhi Kamishna wa
Polisi Benedict, Wakulyamba amesema maandalizi yote yameenda vizuri.
CP. Wakulyamba ameongeza kuwa, kikao hicho ni muhimu kwa
ustawi wa uhifadhi wa Maliasili na Utalii kwa kuwa utaendelea kuimarisha
uwelewa wa pamoja wa Uhifadhi endelevu wa Maliasili na Utalii.
Aidha amewapongeza Maafisa na wataalam wa uhifadhi hapa nchini kwa kushiri
kikamilifu katika maandalizi ya kikao hicho hasa kwa kutanguliza uzalendo
mkubwa kwa maslahi mapana ya wananchi na Taifa kwa ujumla.



0 Maoni