Isimila yang'ara Mkutano wa Kimataifa wa Makumbusho Roma

 

Eneo la kihistoria la Isimila Stone Age Site lililopo katika Mkoa wa Iringa, Tanzania, limetangazwa kushinda miongoni mwa mawasilisho bora ya urithi na utafiti wa pamoja kwenye Mkutano wa Kimataifa wa Makumbusho (International council of museums ICOM 2025) unaofanyika mjini Roma, Italia ulioanza 25-27/9/2025.

Ushindi huo unaonesha thamani ya kipekee ya eneo la Isimila, maarufu kwa zana za mawe yenye zaidi ya miaka 300,000, nguzo za asili na historia yake inayounganisha mabara.

Aidha wasilisho lililowasilishwa pia lilionesha uhusiano na mfanano wa Isimila na Hifadhi ya Taifa Ruaha, ambayo imejaliwa vivutio vya kipekee vya nguzo za asili maarufu kama Magda Natural Pillars.

Kupitia mkutano huo, Tanzania imepata fursa ya kuyatangaza maeneo haya ya urithi duniani kote, kuvutia watafiti wa kimataifa pamoja na wageni wa utalii wa kiutamaduni na kihistoria.

Tanzania kupitia Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) inashiriki kuwasilisha mchango wake wa kulinda urithi huo kwa njia ya ushirikiano, uhifadhi endelevu na ushirikishwaji wa jamii.




Chapisha Maoni

0 Maoni