MAMIA ya
Wananchi wa Kata ya Mwandoya ndani ya
Jimbo la Kisesa, wilayani Meatu wakimsikiliza
Mgombea Mwenza wa Urais wa Chama
Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi wakati akiwahutubia kwenye mkutano wa hadhara
leo Septemba 2, 2025,wakati akiendelea na Mikutano yake ya Kampeni mkoani
Simiyu.
Katika
mkutano huo wa kampeni,Balozi Dk.Emmanuel Nchimbi alimnadi Mbunge wa Jimbo hilo
la Kisesa, Musa Godfrey Mbuga pamoja na diwani wa kata ya Lubiga, Juma Mpina
ambaye ni kaka wa mbunge wa zamani wa jimbo la Kisesa, Luhaga Mpina.
Pamoja na
mambo mengine Balozi Dkt. Emmeanuel Nchimbi amekuwa akiinadi Ilani ya Uchaguzi
Mkuu 2025-2030,ambayo kimsingi imelenga kwenda kuboresha maisha ya wananchi na
ustawi wa Maendeleo katika miaka mitano ijayo huku akitumia nafasi hiyo
kuwaomba wananchi kumchagua mgombea Urais wa CCM Rais Dk.Samia Suluhu,Mgombea
mwenza wa Urais,wabunge na madiwani wa Chama hicho.
0 Maoni