Naibu Katibu
Mkuu OR-TAMISEMI anayeshughulikia Miundombinu Mhandisi Rogatus Mativila yupo
Wilayani Ukerewe kwa ziara ya kikazi.
Katika ziara
hiyo Mhandisi Mativila alipokea taarifa kutoka kwa Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe. Christopher Ngubiagai.
Mhandisi
Mativila ametembelea na kukagua utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa barabara kwa
kiwango cha lami ya RTC-Sungura yenye urefu wa Km 0.321 pamoja na barabara ya
Pump House Km 0.299 katika mji wa Nansio.
0 Maoni