Mgombea
mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha
Mapinduzi (CCM), Dkt. Emmanuel John Nchimbi akiwahutubia Wananchi kwenye
mkutano wake wa hadhara wa
kampeni,uliofanyika leo Septemba 30,2025 katika uwanja wa Kampala-Gongolamboto,Jimbo
la Ukonga wilaya ya ilala,jijini Dar es Salaam.
Akiwa
katika viunga vya Kampala-Ukonga, Dkt. Nchimbi amewahutubia Wananchi huku
akinadi Sera na Ilani ya chama hicho ya 2025-2030 yenye kulenga kuimarisha na
kupeleka maendeleo kwa Wananchi.
Aidha,
baada ya kuhutubia Wananchi, Dkt. Nchimbi pia alipata nafasi ya kuwanadi baadhi
ya wagombea Ubunge wa mkoa huo akiwemo mgombea
Ubunge wa
jimbo la Ukonga,Ndugu Jerry William Silaa, mgombea Ubunge wa jimbo la Kivule
Ndugu Dougras Didas Masaburi na Madiwani.
Dkt. Nchimbi
ni Mgombea mwenza wa Dkt. Samia Suluhu Hassan katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa
kufanyika Oktoba 29, 2025 wakipeperusha bendera ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambapo mkoa wa Dar
es Salaam unakuwa wa 15 kufikiwa na Dkt Nchimbi katika kusaka kura za
ushindi wa Kishindo za Mgombea Urais wa
chama hicho Dkt.Samia Suluhu Hassan,Wabunge pamoja na Madiwani.



0 Maoni