Shirika la Reli Tanzania linatarajia
kuajiri wafanyakazi 2,460 katika mradi wa reli ya kiwango cha kimataifa (SGR)
kwa vipande viwili vya Kutoka Dar es Salaam mpaka Makutopora.
Hayo yamebainishwa wakati wa ziara ya
siku mbili ya bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa reli ya kiwango cha kimataifa (SGR ) na MGR, kati ya Kigoma-Tabora na Tabora
Mwanza iliyoanza Agosti 19, 2025.
Ajira hizo ni mbali na zaidi ya ajira
115,000 ambazo tayari zinatokana na mkandarasi katika kipande cha kwanza mpaka
cha sita.
Katika ajira hizo 2,460 utekekezaji
wake ni awamu ambapo katika mwaka wa
fedha 2024/25 zaidi ya watumishi 500 wameshaajiriwa na mwaka huu wa fedha
2025/26 marajio ni kuajiri watumishi 272 na TRC itaendelea kuajiri kufikia
watumishi 2,460.
Wakati utekekezaji wa utoaji ajira
rasmi za Shirika ukiendelea, jumla ya ajira 115,000 kutoka mkandarasi
zimeshawanufaisha Watanzania 115,000 zikiwemo za vijana wa elimu ya darasa la
saba na viwango vingine vya elimu katika fani mbalimbali.
Mchanganuo wa ajira hizo 115,000
kutoka kwa mkandarasi ni kwamba ajira 35,000 ni za moja kwa moja na
zaidi ya 80,000 ni zisizo za moja kwa moja zikijumuisha makundi mbalimbali kama
baba na mama lishe, bodaboda, bajaji na watoa huduma za makampuni mbalimbali ya
mawasiliano kama mocha, line za simu nk.
Utoaji wa ajira hizo ni utekelezaji wa
maagizo na maelekezo ya serikali kwamba miradi yote ambayo serikali imewekeza
iwe na manufaa kwa Watanzania hususani wale wanaoishi kuzunguka miradi husika
na wengine kutokana na ujuzi unaohitajika kwa viwango vya elimu na ujuzi wao.
0 Maoni