Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la
Kikwajuni, Zanzibar na mtia nia wa ubunge jimbo hilo kupitia Chama Cha
Mapinduzi - CCM, Mhandisi Hamad Yussuf Masauni amemshukuru Rais wa Tanzania
Dkt. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la
Mapinduzi Dkt. Hussein Mwinyi kwa utekelezaji mkubwa wa Ilani ya CCM ya mwaka
2020, suala lililowezesha Jimbo la Kikwajuni na Tanzania kwa ujumla kupiga
hatua kubwa za Kimaendeleo.
Mhe. Masauni amebainisha hayo Agosti
19, 2025 wakati akitoa tathimini ya utekelezaji wa Ilani ya CCM kwenye Jimbo la
Kikwajuni pamoja na ahadi zake mbalimbali, akijivuni kasi kubwa ya maendeleo
iliyopatikana katika huduma mbalimbali za Jamii, ikiwemo Ongezeko kubwa la huduma
ya Maji safi na ya uhakika kwa wananchi pamoja na Ajira kwa Vijana.
"Nichukue fursa hii kuwashukuru
sana Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania,
vilevile na Mhe. Dkt. Hussein Mwinyi, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza
la Mapinduzi kwa kazi kubwa na nzuri waliyofanya na kuweza kufanikisha mambo
mengi sana ya kimaendeleo katika Jimbo langu la Kikwajuni na Tanzania kwa
ujumla. Jimbo langu la Kikwajuni sasa changamoto nyingi zimepungua."
Amekaririwa Mhe. Masauni.
Mhandisi Masauni kadhalika
amewashukuru wananchi wa Kikwajuni kwa ushirikiano mkubwa waliompatia katika
kipindi chote akiwa Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, akisema ushirikiano huo wa
wananchi umekuwa chachu ya kufanikisha utekelezaji wa miradi mbalimbali ya
maendeleo Jimboni humo.
Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Zanzibar na mtia nia wa ubunge jimbo hilo kupitia Chama Cha Mapinduzi - CCM, Mhandisi Hamad Yussuf Masauni amemshukuru Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa utekelezaji mkubwa wa Ilani ya CCM ya mwaka 2020, suala lililowezesha Jimbo la Kikwajuni na Tanzania kwa ujumla kupiga hatua kubwa za Kimaendeleo.
Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Zanzibar na mtia nia wa ubunge jimbo hilo kupitia Chama Cha Mapinduzi - CCM, Mhandisi Hamad Yussuf Masauni amemshukuru Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Mwinyi kwa utekelezaji mkubwa wa Ilani ya CCM ya mwaka 2020, suala lililowezesha Jimbo la Kikwajuni na Zanzibar kwa ujumla kupiga hatua kubwa za Kimaendeleo.
Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Zanzibar na mtia nia wa ubunge jimbo hilo kupitia Chama Cha Mapinduzi - CCM, Mhandisi Hamad Yussuf Masauni akishiriki ugawaji boti za uvuvi katika kutekeleza kipaumbele chake cha ajira kwa vijana.
Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Zanzibar na mtia nia wa ubunge jimbo hilo kupitia Chama Cha Mapinduzi - CCM, Mhandisi Hamad Yussuf Masauni akishiriki ugawaji vyerehani katika kutekeleza kipaumbele chake cha ajira kwa vijana. Pia aligawa bodaboda pamoja na vifaa kwa ajili ya mafundi.
0 Maoni