Manaibu Makatibu Wakuu wa Ofisi ya Rais - TAMISEMI wakiongozwa na
Mhandisi Rogatus Mativila Naibu Katibu
Mkuu (Miundombinu) Sospeter Mtwale - Naibu Katibu Mkuu (TAMISEMI) na Prof.
Tumaini Nagu - Naibu Katibu Mkuu (Afya) wametembea Banda la Wakala ya Barabara
za Vijijini na Mijini (TARURA) katika kilele cha Maonesho ya Sikukuu ya Wakulima Nane Nane katika Viwanja vya
Nzuguni, Jijini Dodoma.
Makatibu Wakuu hao wamepatiwa maelezo mbalimbali kutoka kwa Wataalamu wa
Wakala huo wakiongozwa na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano Bi.
Catherine Sungura kuhusu majukumu, utekelezaji wa miradi mbalimbali pamoja na
mipango ya TARURA inayohusu uboreshaji na ujenzi wa miundombinu ya barabara
nchini.
Akizungumza kwa niaba ya wenzake Naibu Katibu Mkuu Sospeter Mtwale
amewapongeza TARURA kwa kazi nzuri wanayoifanya ya kufungua barabara hususan
maeneo ya wakulima,wavuvi na wafugaji na hivyo kuwarahisishia kusafirisha mazao
yao.
Pia amesema barabara hizo zimesaidia waendesha bodaboda na waendesha
vyombo vya moto vingine na hivyo kupata ajira hivyo kuwataka kuendelea
kuboresha barabara za vijijini ili ziweze kupitika wakati wote.
0 Maoni