WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa leo Oktoba 25, 2025 ni mgeni
rasmi katika kongamano la kilele cha maadhimisho ya miaka 50 ya Taasisi ya
Elimu ya Watu Wazima inayofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha
Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Lengo kuu la kongamano hilo ni kuhakikisha kuwa elimu ya
watu wazima inakuwa chachu ya maendeleo ya kiuchumi, kijamii na kiteknolojia
kwa nchini. Pia ni jukwaa la kubadilishana uzoefu, matokeo ya tafiti na mbinu
bora zinazoweza kuendeleza ubunifu katika utoaji wa elimu ya watu wazima.
Kongamano hilo linalofanyika kuanzia leo tarehe Agosti 25, 2025 hadi Agosti 27, 2025 lina kaulimbiu isemayo Elimu Bila Ukomo kwa Maendeleo Endelevu."
0 Maoni