Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC)
Ndugu. Kailima Ramadhani leo tarehe 30 Agosti, 2025 ameongoza kikao cha
wawakilishi wa vyama vya siasa kupitia na kufanya mabadiliko madogo kwenye
ratiba ya mikutano ya hadhara ya kampeni za wagombea wa Kiti cha Rais na Makamu
wa Rais.
Mikutano hiyo iliyoanza tarehe 28 Agosti, 2025 inaendelea
hadi tarehe 28 Oktoba, 2025 kwa Tanzania Bara na tarehe 27 Oktoba, 2025 kwa
Tanzania Zanzibar.
Uchaguzi wa Rais na Wabunge wa Jamhuri ya Muungano na Madiwani kwa Tanzania Bara utafanyika tarehe 29 Oktoba, 2025.
0 Maoni