Mamlaka ya Usimamizi
wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) inashiriki katika Maonesho ya 49 ya Biashara ya
Kimataifa kwa mwaka 2025 yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Julius K.
Nyerere, vilivyopo barabara ya Kilwa, Jijini Dar es Salaam.
Kupitia maonesho
haya, TAWA inatumia fursa hii kutangaza bidhaa na huduma mbalimbali
zinazohusiana na utalii na uhifadhi zinazotolewa na Mamlaka hiyo.
Unapotembelea banda
la Wizara ya Maliasili na Utalii, utakutana na maofisa wa TAWA ambao watakupa
maelezo kuhusu mambo yafuatayo:
1. Fursa za Uwekezaji
zinazopatikana katika maeneo mbalimbali yaliyo chini ya usimamizi wa TAWA,
ikiwa ni pamoja na:Makuyuni Wildlife Park (Arusha),Pande (Dar es
Salaam),Wami-Mbiki (Morogoro na Pwani),Tabora Zoo (Tabora),Ruhila Zoo (Ruvuma)
na mengine mengi.
2. Fursa ya Kujionea
Wanyamapori Hai kupitia bustani ya wanyamapori iliyopo ndani ya banda la Wizara
ya Maliasili na Utalii, kwa viingilio vya bei nafuu kwa Watanzania.
3. Vivutio vya Utalii
vilivyopo katika maeneo mbalimbali yanayosimamiwa na TAWA, pamoja na taarifa za
gharama na namna ya kuyatembelea.
4. OFA Maalum ya
Ziara ya kutembelea Hifadhi ya Pande, iliyopo Jijini Dar es Salaam, kwa gharama
nafuu katika msimu huu wa Maonesho ya Sabasaba.
5. Shughuli za Utalii
na Uhifadhi zinazofanywa na TAWA, ikiwa ni pamoja na elimu kwa umma kuhusu
namna ya kukabiliana na wanyamapori wakali na waharibifu, na kuelewa tabia zao.
6. Fursa ya Kufurahia
Nyamapori Choma iliyoandaliwa kwa umahiri na kwa kuzingatia ubora wa hali ya
juu Kwa bei ya kizalendo.
Karibuni kwa wingi
katika banda la Wizara ya Maliasili na Utalii, mjifunze, muelimike na mjionee
huduma na vivutio vya kipekee, hasa wanyamapori hai waliopo
ndani ya banda hilo.





0 Maoni