Ofisi ya Msajili wa
Hazina imetoa rai kwa taasisi za umma kutumia maonesho ya 49 ya biashara ya
Kimataifa ya Dar es Salaam maarufu kama
Sabasaba kama jukwaa la kutangaza huduma zinazotolewa na serikali.
Akizungumza Jumatatu,
Julai 1, 2025, katika viwanja vya Sabasaba, Bw. Sabato Kosuri, ambaye ni Kaimu
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano kwa Umma, Ofisi ya Msajili wa Hazina, alisema
wananchi ndio wamiliki wa taasisi za umma na hivyo wanahaki ya kujua uwekezaji
uliofanyika.
Serikali kupitia
Ofisi ya Msajili wa Hazina imewekeza kiasi cha Sh86.25 trilioni katika taasisi
za umma na kampuni ambazo Serikali ina umiliki wa hisa chache.
Kati ya kiasi hicho
Sh83.33 trilioni zimewekezwa kwenye taasisi 152 ambazo serikali ina hisa
nyingi, huku Sh2.82 trilioni zikiwekezwa kwenye kampuni 56 ambazo serikali ina
umiliki wa hisa chache.
Bw. Kosuri alisema
Maonesho ya biashara ya Sabasaba ni mwendelezo wa tafsiri ya ndoto ya Mhe. Rais
Dk. Samia Suluhu Hassan katika kuongeza ufanisi wa taasisi za umma lengo likiwa
ni kuleta tija na rejesho halisi la uwekezaji uliofanywa katika taasisi za
umma.
“Sisi kama wasaidizi
wa Mhe. Rais tumedhamiria kutengeneza mazingira ya uwajibikaji kwani taasisi za
umma ni mali za umma na hivyo
zinawajibika moja kwa moja kwa umma,” alisema.
Bw. Kosuri alisema
ushiriki wa Ofisi ya Msajili wa Hazina na taasisi inazozisimamia katika
maonesho ya Sabasaba utawapa fursa kwa wadau na wananchi kwa ujumla kuuliza
maswali na kutoa maoni.
“Tutumie maonesho ya
Sabasaba kama jukwaa la kupokea maoni na kuwaambia wadau na wananchi kwa ujumla
mambo ambayo serikali ya awamu ya sita chini ya Mhe. Rais. Dk. Samia Suluhu
Hassan inayafanya,” alisema Bw. Kosuri.
ili kuzungumza na wadau na wananchi pamoja na
kupokea maoni pamoja na kuwaelezea mambo yaliyo na yanayotekelezwz na serikali
ya awamu ya sita.
Alihitimisha kwa
kuwakaribisha wadau mbalimbali na wananchi wote katika banda namba 39 la Ofisi
ya Msajili wa Hazina lililopo katika
ukumbi wa Kilimanjaro.
0 Maoni