Wataalam wa Wizara ya
Nishati pamoja na taasisi zake wameshiriki katika Mkutano wa ngazi ya
Makatibu Wakuu na Watalaam wanaoshughulikia masuala ya Nishati na Maji
unaofanyika katika Jiji la Harare nchini Zimbabwe.
Mkutano huo wa awali ulioanza jana ni sehemu ya maandalizi kuelekea katika Mkutano wa pamoja wa Kamati ya Mawaziri
wanaoshughulikia masuala ya Nishati na Maji wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa
Afrika (SADC).
Mkutano huo pamoja na
kujadili masuala ya Nishati na Maji, umekuwa ni fursa pia kwa Tanzania kuendeleza diplomasia ya kiuchumi pamoja na
kuwasilisha mafanikio ya nchi katika kuboresha huduma za nishati vijijini
kupitia miradi inayotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijjni (REA).
Aidha, Mkutano huo
umeangazia maendeleo ya Sekta ndogo ya Mafuta na Gesi, pamoja na ujenzi wa
miundombinu ya kikanda ya Mafuta na gesi inayohusu nchi wanachama wa SADC.
Wataalam kutoka
Wizara ya Nishati na taasisi zake waliohudhuria mkutano huo ni Kamishna
Msaidizi wa Maendeleo ya Umeme, Mha. Styden Rwebangila, Mkurugenzi Mkuu wa REA,
Mha. Hassan Saidy, Mkurugenzi wa Mipango
na Uwekezaji (TPDC), Derick Moshi, Mkurugenzi wa Mifumo ya Udhibiti Umeme
(TANESCO) , Mha. Deogratius Mariwa, Mkurugenzi wa Udhibiti Uchumi (EWURA),
Msafiri Mtepa na Wataalam kutoka Wizara
ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
0 Maoni