Kamishna wa Uhifadhi
wa Mamlaka ya Hifadhi ya eneo la Ngorongoro (NCAA) Bw. Abdul-Razaq Badru
kupitia mkutano na Waandishi wa Habari uliofanyika jana jijini Arusha tarehe 30
Juni, 2025 amewashukuru Watanzania, Wadau wa Sekta ya Utalii na wageni
mbalimbali waliotembelea eneo la hifadhi ya Ngorongoro kwa kuipigia Kura
hifadhi hiyo na kuiwezesha kutangazwa kuwa Kivutio bora cha Utalii Barani
Afrika mwaka 2025.
Hafla ya kutangaza
washindi wa tuzo hizo zinazoratibiwa na
Mtandao wa World Travel Awards (WTA) ilifanyika tarehe 28 Juni, 2025
Jijini Dar es Salaam.



0 Maoni