Mkuu wa Mkoa wa Lindi
Mhe. Zainab Telack amesema Serikali inatambua mchango wa Mashirika Yasiyo ya
Kiserikali katika kuleta maendeleo kwa wananchi.
Hayo yamesemwa mkoani
Lindi kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa huo na Mkuu wa Wilaya ya Linda Mhe. Victoria
Mwanziva wakati akifungua Jukwaa la Mwaka la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali
mkoani humo.
Mhe. Victoria amesema
Serikali inatambua mchango wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kwani ni muhimu
katika kuhakikisha mipango ya Serikali inatimia ya kuwahudumia wananchi katika
maeneo mbalimbali kupitia sekta mbalimbali zenye kuigusa jamii.
"Niseme kuwa NGOs ni
mkono wa pili wa Serikali katika kuleta maendeleo kwa jamii hivyo tutaendelea
kuweka mazingira mazuri na wezeshi ya kufanya kazi zenu na kutekeleza miradi
mbalimbali." amesema Mhe. Victoria
Ameongeza kuwa Mashirika
hayo yanatakiwa kufanya zao kwa kuzingatia Sheria na taratibu zilizopo ikiwemo
kutekeleza matwajanya Sheri ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kwa kuhakikisha
wanatoa taarifa zao za robo Mwaka na Mwaka na mikataba ya kifedha katika
utekelezaji wa miradi mbalimbali.
"Tufuate Sheria na
Kanuni zilizopo katika utekelezaji wa majukumu yetu haswa katika kufanya kazi
na Mamlaka ambazo tunafanya kazi zetu mfano Afya, Maji, Elimu, Mazingira na
Sekta zingine ili tuwe na uratibu mzuri wa utekelezaji wa miradi,"
amesisitiza Mhe. Victoria.
Kwa upande wake
Mwakilishi wa Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kutoka Wizara ya
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Fransisca Mwendesha
amesema Serikali inatambua kazi kubwa ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali katika
kuwahudumia wananchi ila ameyataka Mashirika hayo kuendelea kuzingatia Sheria
taratibu zilizopo ili waweze kuwa katika mazingira mazuri ya Utekelezaji wa
majukumu yao.
Naye Mwenyekiti wa Baraza
la Taifa la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NACoNGO) Jasper Makala amesema
Baraza hilo linaendelea kuwa kiungo muhimu katika ya Sekta ya NGOs na
Serikali,hivyo amewaomba Mashirika hayo kuendelea kuzingatia Sheria taratibu
zilizopo katika utekelezaji wa majukumu ili kutimizaalengo ya Shirika na
Serikali kwa ujumla.
Majukwaa ya Mashirika
Yasiyo ya Kiserikali kuanzia ngazi ya Halmashauri mikoa na Taifa yanaongozwa na
Kaulimbiu isemayo: Tathmini ya Mchango wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali katika
Maendeleo ya Taifa 2020/2021-2024/2025; Mafaniko, Changamoto, Fursa na Matarajio.
0 Maoni