Mshambuliaji wa
Liverpool, Diogo Jota, amefariki dunia katika ajali ya gari nchini Hispania
baada ya gari lake kutoka barabarani kufuatia kupasuka kwa tairi alipokuwa
akipita gari jingine, kwa mujibu wa polisi wa eneo hilo.
Ndugu yake, Andre
Silva, naye pia alipoteza maisha kwenye ajali hiyo. Jota, mwenye umri wa miaka
28, alifunga ndoa na mchumba wake mwezi uliopita, walikuwa na watoto watatu
pamoja.
Mchezaji huyo wa
kimataifa wa Ureno alikuwa sehemu muhimu ya kikosi cha Liverpool kilichoshinda
Ligi Kuu ya England msimu uliopita.
Timu ya taifa ya
Ureno imesema Jota hakuwa tu "mchezaji wa kipekee" bali pia "mtu
wa aina yake aliyekuwa akiheshimika na wachezaji wenzake wote pamoja na wapinzani
wake."



0 Maoni