Matukio mbalimbali katika maonesho ya biashara ya dunia yanayoendelea katika Jiji la Osaka, nchini Japan (EXPO 2025, Osaka).
Tanzania imeshiriki katika maonesho hayo ambapo juma la Kiswahili
na utamaduni linaendelea na ifikapo Julai 7, 2025, Tanzania itafanya
maadhimisho ya Siku ya Kiswahili Duniani (MASIKIDU) hapa Osaka katika maonesho
ya biashara ya dunia yanayoendelea katika Kisiwa cha Yumeshima, Osaka.
Maadhimisho ya Siku ya Kiswahili kikanda (Afrika Mashariki)
yanatarajiwa kufanyika nchini Rwanda na kwa Tanzania, maadhimisho hayo
yatafanyika visiwani Zanzibar.




0 Maoni