Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe. Mohamed
Mchengerwa amemtaka mkandarasi anayetekeleza
Mradi wa Barabara ya Banana – Kitunda – Kivule – Msongola na Kivule –
Majohe Junction, barabara za Kiwalani na Migombani kukamilika mradi huo kwa
wakati bila kutoa visingizio vyovyote kwa kuwa tayari Serikali imeshamlipa
fedha zote.
Mhe. Mchengerwa ametoa
kauli hiyo leo wakati akikagua mradi huo akiambatana na Mbunge wa jimbo la
Ukonga Mhe. Jerry Silaa.
Amesema dhamira ya
Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan ni kuhakikisha kuwa miundombinu ya
barabara zote nchini inakamilika ili ziweze kupitika katika kipindi chote cha
mwaka.
Aidha, amefafanua kuwa
kukamilika kwa ujenzi wa barabara utasaidia kuboresha maisha ya wananchi kwa kuwa shughuli za uchumi
zutaimarika.
Amempongeza Mhe. Rais kwa
kutoa fedha nyingi kutengeneza miradi mbalimbali ya barabara hapa nchini huku
akizitaka Mamlaka za Mikoa na Wilaya kuwasimamia wa wahandisi wanaotekeleza
miradi hiyo na wasisite kuwazingatia mikataba ya kazi hizo.
Akitoa maelezo ya mradi
huo, Meneja wa TARURA Mkoa wa Dar es Salaam Mhandisi Geofrey Mkinga amesema ujenzi
wa barabara ya Banana- Kitunda- Kivule –Msongola unafanywa kwa awamu 2 tofauti
ya 1 & 2 Mkandarasi M/s JIANGXI GEO ENGINEERING.
Utekelezaji kwa awamu ya
kwanza ya mradi unahusisha ujenzi wa
barabara ya Kitunda – Kivule – Msongola yenye urefu wa km 9.95 na barabara ya
Kivule – Majohe Junction km 2.79 unaotekelezaji unafanywa na M/s JIANGXI GEO
ENGINEERING chini ya usimamizi wa Mhandisi Consultancy Ltd.
Amesema mradi
unatekelezwa kwa fedha za Mkopo kutoka Benki ya Dunia, kwa gharama ya TSh 30.37
bilioni.
Aidha, amesema malipo
yaliyokwishafanyika hadi sasa ni TSh. 4.55 bilioni kama malipo ya awali.
Hadi kufikia leo, mradi
umefikia hatua ya utekelezaji ya 10%, huku muda wa utekelezaji uliopita ukiwa
ni 32%.
Ameongeza kuwa kazi
zilizokamilika ni pamoja na uondoaji wa tabaka la juu la udongo usiofaa
kwa kilomita 5,
ujenzi wa msingi wa
barabara (roadbed) kwa kilomita 4, uwekaji wa vifusi aina ya G3 kwa kilomita 3
na uwekaji wa vifusi aina ya G7 kilomita
4.
Kwa upande wautekelezaji
wa awamu
ya pili amesema Mradi unahusisha ujenzi wa barabara ya Banana -Kitunda
yenye urefu wa km 3.95, barabara ya Migombani km 1.57, barabara na barabara za
Kiwalani zenye urefu wa km 3.22.
Aidha amesema utekelezaji
unafanywa na M/s JIANGXI GEO ENGINEERING chini ya usimamizi wa Mhandisi
Consultancy Ltd.
Mradi unatekelezwa kwa
fedha za Mkopo kutoka Benki ya Dunia, kwa gharama ya TSh 28.51 bilioni.
Amesema kazi
zilizokamilika ni pamoja na kazi za Survey kwa kuweka mipaka na vipimo vya
barabara zote.
Aidha, amesema changamoto iliyojitokeza katika mradi
huo ni mvua nyingi zilizonyesha kuanzia
Februari hadi Juni 2025, ambazo ziliathiri kuanza kwa kazi nyingi ndani ya muda
uliopangwa na uwepo wa wafidiwa katika kipande cha barabara ya Banana-Kitunda
eneo la Kipunguni ambao bado hawajapokea malipo yao. (Ulipwaji wa fidia hiyo
unafanywa na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege-TAA ikiwa ni kupisha eneo la Uwanja
wa Ndege).
Pamoja na kwa Packages
zingine ambazo fidia yake bado haijafanyika ili kupisha
kuanza utekelezaji.
Na. John Mapepele - Dar
es Salaam
0 Maoni