WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa leo Julai 04, 2025
amemwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katik maadhimisho ya miaka kumi ya
Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), katika kituo cha Mikutano cha Kimataifa
cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Maadhimisho hayo yana lengo la kutathmini mafanikio
yaliyofikiwa katika kipindi cha miaka kumi, kuonesha mshikamano kati ya wadau
na kuweka mikakati ya kuboresha huduma za fidia kwa wafanyakazi nchini.
Kaulimbiu ya maadhimisho hayo ni Miaka kumi ya Fidia kwa
Wafanyakazi-Kazi Iendelee
0 Maoni