Viongozi wa dini
mbalimbali Hospitali ya Taifa Muhimbili wamekutana na Mkurugenzi mpya wa
Shirika la Afya Duniani (WHO) Kanda ya Afrika, Profesa Mohamed Janabi, kwa
lengo la kumpongeza, kumuaga rasmi, pamoja na kuliombea taifa la Tanzania
amani, mshikamano na uongozi bora.
Viongozi hao kutoka
madhehebu ya Kikristo, Kiislamu na mengineyo, wameungana na watumishi wa
hospitali hiyo na kuonesha mshikamano wao katika kumuaga Prof. Janabi, ambaye
kwa miaka mingi ametoa mchango mkubwa katika sekta ya afya nchini.
Katika hatua
nyingine, viongozi hao wa dini wameomba dua na sala kwa ajili ya taifa la
Tanzania, wakilitakia amani, umoja na maendeleo endelevu pamoja kumuombea
Profesa Janabi baraka na hekima katika majukumu yake mapya.
Profesa Janabi
amechaguliwa kuwa Mkurugenzi wa Kanda ya Afrika wa Shirika la Afya Duniani
(WHO), Mei 18 mwaka huu na anatarajiwa kuanza kazi rasmi katika makao makuu ya
WHO Kanda ya Afrika, yaliyoko Brazzaville, Jamhuri ya Congo, ambapo atakuwa na
jukumu la kuratibu na kuongoza sera za afya kwa nchi wanachama wa bara la
Afrika.
0 Maoni