WAZIRI MKUU, Kassim
Majaliwa ameitaka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na TAMISEMI pamoja
kusimamia na kudhibiti ubora wa elimu inayotolewa kuanzia elimu ya msingi mpaka
elimu ya juu ili kuendelea kukidhi viwango vya kitaifa, kikanda na kimataifa.
Ametoa maagizo hayo
leo (Ijumaa Juni 20, 2025) alipomwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye
maadhimisho ya miaka 20 ya Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro (MUM), kwenye
viwanja vya chuo hicho mkoani Morogoro.
“Mamlaka zetu
ziendelee kusimamia hilo kwa kufanya hivyo sio tu kutaendelea kukuza ubora wa
elimu yetu, bali pia kutawawezesha wasomi nchini kukidhi viwango na mahitaji ya
soko la ajira.”
Kadhalika, Mheshimiwa Majaliwa amezitaka
Taasisi za Elimu nchini ziimarishe mahusiano na vyuo vyote nchini vinavyotoa
maarifa kwa vijana wa kitanzania pamoja na kuzalisha wakufunzi ili kuwa sehemu
ya mtandao wa utoaji maarifa na taalum hapa nchini.
Aidha, Mheshimiwa
Majaliwa kuwa katika kuunga mkono jitihada za wadau mbalimbali katika kuchangia
maendeleo ya chuo hicho kupitia mfumo maalum wa (MUM Community Fund), Rais Dkt.
Samia ametoa kiasi cha Shilingi milioni 100 ili kiendelee kutoa huduma kwa
watoto wa Kitanzania.
Mheshimwa Waziri Mkuu
ameongeza kuwa Serikali inaendelea na ujenzi wa Mfumo wa Takwimu wa Sekta ya
Elimu utakaowezesha upatikanaji wa takwimu zote za sekta hiyo ambao utakuwa na
uwezo wa kupokea takwimu mbalimbali zinazohusiana na elimu kutoka katika mifumo
mingine ya Serikali ikiwemo NIDA, RITA na Wizara ya Mambo ya Nje.
Kwa Upande wake Naibu
Waziri wa Elimu Qs Omar Kipanga amesema kuwa katika kipindi cha miaka 20, chuo
hicho kimefanikiwa kuwa na progrma zaidi ya 32 kutoka program mbili wakati
kinaanza na kimefanikiwa kutoa wahitimu zaidi ya 15,000.
“Wahitimu hawa
wamekuwa wwamekuwa wa kupigiwa mfano katika kazi na maadili inayofanya
waaminiwe katika nafasi mbalimbali kwenye jamii na Serikali kaa ujumla.”
Kadhalika, ameongeza
kuwa Chuo hicho kimeweka mipango inayozingatia dira ya maendeleo ya Taifa ya
2050 na mwelekeo mpya wa Elimu Nchini Tanzania unaolenga kutoa Elimu Ujuzi,
Stadi na Maarifa kwa ajili ya kuwajengea wahitimu uwezo na sifa za kujiajiri na
kuajirika katika soko shindani la ajira duniani.
Naye Mufti na Sheikh
Mkuu wa Tanzania Sheikh Dkt. Abubakar Zubeir bin in Ali ametoa wito kwa Waislam
na Watanzania kwa ujumla kuweka mikakati ya kukisaidia chuo ili kiendelee
kufanya vizuri na kutoa elimu kwa watanzania nchini.
“Waislam na
watanzania tukisaidie chuo hichi, hakuna uislam bila ualimu, uislam ulipokuja
ulipiga sana vita ujinga, tuwaunge mkono viongozi wetu kwa kukisaidia chuo hiki.”
Makamu Mkuu wa Chuo
hicho Prof Juma Assad amesema kuwa moja ya changamoto kubwa katika chuo hicho
ni kukosekana kwa hosteli za wanafunzi wa kike “Namna tunavyoingeza udahili
ndivyo tunavyoibua changamoto nyingine, tunataka watoto wetu wa kike wote
wake ndani ya chuo.”
0 Maoni