Naibu Katibu Mkuu
Ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia afya Prof. Tumaini Nagu amewaelekeza
Waganga Wakuu wa Mikoa (RMO’s) kuhakikisha wanasimamia upatikanaji wa ithibati
katika maabara za hospitali zote za Halmashauri zilizopo katika Mikoa yao.
Prof. Nagu ametoa
maelekezo hayo wakati wa kikao cha majumuisho wa ziara yake ya usimamizi
shirikikishi katika Mkoa wa Pwani kilichofanyika katika Halmashauri ya mji wa
kibaha mkoani hapo.
“Ithibati ndio alama
ya ubora, ukiwa nayo maana yake wewe umekidhi vigezo hivyo huduma zako ni bora,
hivyo tunaanza na maabara zote katika ngazi ya afya msingi kuhakikisha tunapata
ithibati ya ubora wa huduma zetu,” amesisitiza.
Aidha, Prof. Nagu
amewataka watumishi kutoa huduma zenye ubora kwa kuzingatia miongozo (SOP) ya
utoaji wa huduma katika maeneo ya kazi.
“Lazima tuzingatie
miongozo ya utoaji wa huduma. Hivyo naelekeza standard operation procedures
(SOP’s) zipatikane katika maeneo husika na zitumike kuhakikisha huduma
zinazotolewa ni bora. Aidha, vifaa kinga (PPEs) zipatikane na zitumiwe na watoa
huduma hususani katika maeneo kama ya kutakasia nguo, maabara, chumba cha
kuhifadhi maiti pamoja na maeneo ya kuchoma taka” amesema Prof. Nagu.
Prof. Nagu pia,
ameelekeza upimaji wa maeneo yote ya kutolea huduma za afya na kupata hati ya
umiliki wa aridhi ili kuondoa changamoto ya migogoro ya ardhi.
Na. OR - TAMISEMI



0 Maoni